Kiungo mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi aliyekuwa majeruhi amejumuishwa katika kikosi kilichoelekea visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi.
Mahadhi amekuwa nje kwa zaidi ya miezi minne akiuguza majeraha ya goti.
Mwezi uliopita alianza mazoezi mepesi ikiwa ni program maalum ya kumrejesha dimbani.
Mahadhi mmoja wa wachezaji wanaotabiriwa kuwa na mafanikio baadae , huenda akapata nafasi ya kurejea dimbani na kulicheza gozi la n'gombe baada ya kupona majeraha yake
ADVERTISE HERE