Kutokana na kasi yake ya kuzifumania nyavu, mshambuliaji kinara wa mabao ligi kuu ya Tanzania Bara Heritier Makambo anaweza kufikisha mabao 30 msimu huu.
Makambo anaongoza orodha ya wapachika mabao ligi kuu ya Tanzania Bara akiwa amefunga mabao 11 katika michezo 17 aliyocheza.
Mcongoman huyo alifunga mwaka 2018 kibabe kwa kupachika mabao yote mawili ya Yanga kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City.
Makambo amekuwa katika kiwango bora zaidi cha kuzifumania nyavu na mabao yake yamechangia kwa kiasi kikubwa kuifanya Yanga iongoze ligi ikiwa na alama 50
Amedhihirisha kuwa ni mshambuliaji aliyekamilika kwani amekuwa akifunga mabao ya kila aina.
ADVERTISE HERE