Kwa Yanga, mikoani ni kwepesi kuliko Dar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jan 2019
Kwa Yanga, mikoani ni kwepesi kuliko Dar

Wakati Yanga ilipocheza mechi nyingi jijini Dar es salaam na kupata matokeo, wapo waliotabiri kuwa mabingwa hao wa kihistoria Tanzania 'watapata tabu sana' watakapoanza kucheza mikoani.

Hata hivyo ile kauli ya kocha Mwinyi Zahera kuwa Yanga itakuwa hatari zaidi huko mikoani imedhihirika baada ya vinara hao wa ligi kushinda michezo yao yote waliyocheza nje ya jiji la Dar es salaam.

Ushindi wa mikoani ulianza kama utani kwa kuichapa Mwadui Fc mabao 2-1, kisha Kagera Sugar nayo ikachezea kichapo kama hicho.

Tanzania Prisons ikapigwa mabao 3-1 kabla ya kufika zamu ya African Lyon iliyolazwa kwa bao 1-0 jijini Arusha.

Juzi Yanga ikafunga mwaka 2018 kibabe kwa kuichapa Mbeya City mabao 2-1 katika mchezo ambao wapinzani wa Yanga walitaraji ingepoteza pointi mkoani Mbeya.

Jana Zahera aliwaambia waandishi wa habari kuwa timu yake inapocheza ugenini inakuwa na utulivu zaidi kuliko inapocheza nyumbani.

"Unapocheza nyumbani unakuwa na presha ya kutaka kushinda ambayo inaweza kuufanya mchezo kuwa mgumu zaidi, lakini unapokuwa ugenini unacheza bila ya presha."

"Lakini pia sisi tulijiwekea malengo kuwa ushindi ndio kipaumbele cha kwanza kwenye kila mchezo tunaocheza bila ya kujali tuko nyumbani au ugenini."

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
2h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’