Katika Mkutano na Waandishi wa habari ulioandaliwa jana na Yanga, mkongwe Sunday Manara alipata nafasi ya kutoa salamu za shukrani kwa kocha Mwinyi Zahera baada ya kikao walichokaa nae.
Manara ambaye ni baba mzazi wa msemaji wa Simba (Haji), mbali na kumpongeza Zahera, amesema kwa mafanikio iliyopata Yanga mpaka sasa anaamini uwezekano wa kufanya vizuri zaidi na hata kutwaa ubingwa msimu huu ni mkubwa
"Tumempongeza Zahera kwa kazi nzuri anayofanya na tumekutana nae ili kumuhakikishia kuwa sisi wachezaji wa zamani tuko nae bega kwa bega," amesema Manara
"Licha ya kukabiliwa na hali ngumu ya kipesa, Zahera amefanya kazi nzuri pamoja na wachezaji ambao nao tunawapongeza kwani wameonyesha bidii isiyo ya kawaida"
"Pia tunawapongeza viongozi wa Yanga kwa kazi kubwa waliyofanya kuendelea kuifanya Yanga iwe moja licha ya kukumbwa na misukosuko ya hapa na pale"
"Kwa hali ilivyo sasa tumewasha indiketa, naamini msimu huu tutafika mbali"
Wakongwe hao wameahidi kuendelea kushirikiana na uongozi kwa kuandaa utaratibu nzuri zaidi ambao utakuwa na manufaa kwa Yanga