Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amefichua kuwa kikao chake na wachezaji wa zamani wa timu hiyo kilichofanyika leo Makao Makuu ya klabu hiyo kilikuwa na manufaa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Zahera amesema wakongwe hao walimueleza mambo mengi mazuri na ameshauri utaratibu huo uendelezwe.
"Nimefurahi kuonana nao kwani wamenieleza mambo mengi mazuri.. Ushirikiano huu utatusaidia kufika mbali zaidi. Ili tupate mafanikio ni vyema kusikiliza ushauri wa wengine," amesema
Aidha Zahera amegusia kuwa katika mijadala yao yote hakukuwa na ajenda iliyomuhusu mlinda lango Beno Kakolanya.
"Hatukuzumza mambo ya Beno. Mjadala wake tumeshaufunga"
ADVERTISE HERE