Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema anakusudia kuwapumzisha baadhi ya wachezaji katika michuano ya kombe la Mapinduzi inayoanza kesho visiwani Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Zahera amesema kutokana na michuano mingi kuikabili Yanga mwezi Januari 2019, anaona ni vyema kuwa na kipaumbele
"kufuatana na nguvu yetutulionayo inatubidi tuangalie wapi tutapata faida,tupo na ligi kuu,tupo na Azam federation cup, Mapinduzi cup na Sport Pesa," amesema
"Inabidi sisi kama yanga tuwe na malengo kwenye kitu chenye manufaa kwetu tukiamua kuyataka makombe yote tunaweza kosa yote ivyo lazma baadhi ya wachezaji wapumzike kwaajili ya ligi na ASFC"
Ukiacha kombe la Mapinduzi,mwishoni mwa mwezi wa kwanza Yanga inakabiliwa na mashindano ya Sportpesa Super Cup.
Pia baada ya Mapinduzi Cup kumalizika Jan 12, ratiba ya michezo ya ligi na kombe la FA (ASFC) itaendelea kama kawaida