Ni zaidi ya wiki mbili zimepita tangu kiungo Mcongoman Papi Kabamba Tshishimbi alipoaga kwenda kwao Congo kuhudhuria msiba wa mkwe wake.
Hata hivyo inaelezwa kiungo huyo ambaye alitakiwa awe amerejea, hajawasiliana na viongozi wa Yanga na simu yake imekuwa haipatikani jambo linaloibua maswali mengi.
Moja ya mambo ambayo Zahera amekuwa akiyapigia kelele kuwa hayataki kwenye timu yake ni hili la wachezaji kutokuwa kikosini bila ya kutoa sababu za msingi.
Msimu huu umekuwa mgumu sana kwa Tshishimbi ambaye usajili wake msimu uliopita ulikuwa na faida kubwa kwa Yanga kutokana na kiwango kikubwa alichoonyesha.
Lakini sasa Tshishimbi amekuwa akicheza chini ya kiwango suala la majeraha ya mara kwa mara likitajwa kuwa sababu
Mkataba wa Mcongoman huyo unamalizika mwishoni mwa msimu na atakaporejea huenda akalazimika kufanya kazi ya ziada kurejea kwenye kikosi cha kwanza hasa baada ya usajili wa Haruna Moshi 'Boban' ambaye juzi Zahera alimsifu kuwa anafanya kile anachomuelekeza.
Zahera amewahi kumkosoa Tshishimbi kuwa anafanya mambo mengi sana uwanjani yanayomfanya achoke na kushindwa kuisaidia timu