Mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya Azam Fc dhidi ya Yanga ambao awali ulipangwa kupigwa Januari 03 2019 umeahirishwa kuzipa nafasi timu hizo kwenda kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi inayoanza keshokutwa, Januari 01 2019 visiwani Zanzibar.
Hata hivyo Azam na Yanga zimepangwa kundi moja (B) na zitakutana kwenye michuano hiyo itakayomalizika Januari 12 2019.
Yanga itashuka dimbani Januari 03 kucheza na KVZ na siku mbili baadae, Januari 05 itachuana na Azam FC.
Bingwa wa michuano hiyo atatwaa kombe na kitita cha Tsh Mil 15.
Mwaka huu michuano hiyo inashirikisha timu za Tanzania pekee baada ya URA kujitoa
ADVERTISE HERE