Msanii maarufu Christian Bella raia wa DR Congo jana alikuwepo uwanja wa Sokoine kumuunga mkono Mcongoman mwenzie Heritier Makambo aliyekuwa shujaa wa mchezo dhidi ya Mbeya City
Makambo alifunga mabao yote mawili ya Yanga kwenye ushindi wa mabao 2-1 na kuifanya Yanga ijikite kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 10 baada ya kufikisha alama 50.
Bella alianzisha 'amshaamsha' dimbani huku akitumia staili ya ushangiliaji ya Makambo na kuibua furaha kwa mashabiki wa Yanga waliokuwa wamefurika uwanja wa Sokoine.
Hata baada ya mchezo Bella aliyekuwa na marafiki zake wenye asili ya Congo waliendelea kushangilia huku wakimsifu na kutaja jina la Makambo
ADVERTISE HERE