Mashabiki wa Yanga Mbeya wawajaza mapesa wachezaji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Dec 2018
Mashabiki wa Yanga Mbeya wawajaza mapesa wachezaji

Utaratibu wa mashabiki na wanachama wa klabu ya Yanga kuichangia timu hiyo kila mkoa inaokwenda umeanza kuwa na manufaa kwa vinara hao wa ligi kuu baada ya leo mkoani Mbeya wachezaji na benchi la ufundi kupewa posho kabla ya mchezo dhidi ya Mbeya City.

Posho hizo ni fedha zilizochangiwa na Wana Yanga wa mkoa wa Mbeya na wale wa mkoa wa Songwe ambao wamejumuika na wenzao wa Mbeya kuhakikisha Yanga inapata ushindi dhidi ya Mbeya City leo.

Aidha Wana Yanga hao wameurasimisha utaratibu wa mashabiki kuichangia timu uwanjani baada ya kutengeneza 'kontena' maalum za kukusanyia michango hiyo.

Utaratibu huu ulianzishwa na mashabiki wa Yanga wa mkoa wa Arusha wakati Yanga ilipokwenda kucheza na African Lyon.

Wana Yanga wa Mbeya na Songwe wanastahili pongezi kwa jitihada zao na hakika hiyo ndio maana halisi ya timu ya Wananchi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’