Timu ya Wanawake ya Yanga inayotambulika kwa jina la Yanga Princess imepata ajali mkoani Kigoma ilikokwenda kucheza mchezo wa ufunguzi wa ligi ya Wanawake inayotarajiwa kuanza kesho.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na uongozi wa Yanga, ajali hiyo imetokea Uvinza.
"Ikiwa safarini kuelekea Kigoma, timu yetu ya wanawake (Yanga Princes) imepata ajali maeneo ya Uvinza," imesema taarifa ya Yanga
"Kwa mujibu wa taarifa, basi lililobeba wachezaji hao liliacha njia na kuelekea porini kufuatia kona Kali, hakuna mtu aliyepoteza maisha lakini baadhi ya wachezaji wamepata majeraha"
Tunawapa pole wote walodhurika, Tunawaombea wapone haraka majeraha yao ili waweze kurejea kuitumikia klabu ya Yanga
ADVERTISE HERE