Kocha wa klabu ya Yanga Mwinyi Zahera amesema klabu hiyo ataendeleza historia ya kuondoka na ponti tatu mikoani pale wanapokutana na timu pinzan iwakati watakaupokutana na Mbeya City kesho.
Zahera ametamba hivyo leo baada ya kumaliza kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa.
βSisi mwendo wetu ni uleule wa kuondoka na pointi tatu ni kila mechi tutakayocheza.
"Yote hiyo ni kwa sababu kikosi changu ni kizuri hivyo nawaomba mashabiki wa Yanga waje kwa wingi na kushuhudia tunaitandika Mbeya City kwenye uwanja wao wa nyumbaniβ, alisema Zahera.
Zahera ameongeza kuwa anatarajia kuona marefa watakao chezesha mchezo wao wa kesh watakuwa na weledi wa hali ya juu katika kutafsiri sheria za mpira wa miguu.
Hata hivyo Zahera amesema katika mchezo wa kesho anatarajia kumchezesha Haruna Moshi maarufu Bobani kutokana kupendezwa na mchezo wake aliyouonyeshwa wakati wa mechi ya Tukuyu star uliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.