Vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara, Yanga wako mkoani Mbeya wakijiwinda na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City
Mchezo huo utapigwa kesho Jumamosi, Disemba 29 kwenye uwanja wa Sokoine
Mabingwa hao wa kihistoria walitua mkoani Mbeya mapema jana na kufikia Hotel yenye hadhi ya nyota tano, FQ Hotel.
Leo asubuhi wamejifuajifua katika uwanja wa JKT Itende kujiandaa na mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.





ADVERTISE HERE