Ligi ya Wanawake kuanza Jumamosi, Yanga Princess kushiriki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Dec 2018
Ligi ya Wanawake kuanza Jumamosi, Yanga Princess kushiriki

Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Premium Lite inatarajia kuanza Jumamosi ya Desemba 29, 2018 ikishirikisha timu 12 kwa mfumo wa nyumbani na ugenini.

Akizungumza mapema leo kuelekea kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Serengeti Premium Lite, Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake Amina Karuma amesema msimu huu utakua na ushindani mkubwa.

Amesema kwa namna timu zote zilivyojiandaa na kwa udhamini wa kinywaji cha Serengeti Lite,inaifanya ligi kuongeza ushindani zaidi.

“Ni ukweli usiopingika kwamba ligi yetu ya wanawake ambayo inadhaminiwa na Serengeti Premium Lite inaongezeka chachu ya ushindani na tunatarajia msimu unaoanza utakua na ushindani zaidi” amesema Karuma.

Kwa upande wake, Afisa masoko wa Serengeti Breweries Bw. George Mango amesema wamejiandaa vya kutosha kuwezesha mashindano hayo kuonesha msisimko ili kuwapatia burudani mashabiki wa mpira wa miguu pamoja na kutoa ushindani mkubwa wa soka la wanawake kupitia bia murua ya Serengeti Premium Lite.

“Serengeti Breweries Limited kupitia kinywaji chake cha Serengeti Premium Lite imewekeza kiasi cha Shilingi milioni 450 ili kuwezesha ligi hii ya wanawake iwe ya ushindani mkubwa na kuwaletea msisimko mashabiki wa soka hapa nchini,” alisema George na kubainisha kwamba maandalizi ya kuwezesha michuano hiyo yamekamilika.

“Watanzania wakae tayari sasa kuona burudani maridhawa kutoka kwa timu zinazoshiriki ligi hii. Hakika ni ligi inayotarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu sana,” alisema.

“Tumeona namna ambavyo ligi ilivyoweza kutoa misisimko na msimu huu timu zimeongezeka kutoka 8 kwenye ligi mwaka jana hadi 12 za sasa”

Timu 12 zitakazoshiriki ligi hiyo ni Kigoma Sisters ya Kigoma, JKT Queens, Simba Queens, Yanga Princess, Evergreen za Dar es Salaam, Alliance Girls, Marsh Academy za Mwanza, Baobab Queens ya Dodoma, Mlandizi Queens ya Pwani, Panama ya Iringa, Mapinduzi Queens ya Njombe na Tanzanite ya Arusha

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
44m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’