Kiungo wa Yanga Mohammed Issa 'Banka' amefichua kuwa atatumia jezi namba nane wakati atakapoanza rasmi kuitumikia Yanga mwezi Februari 2019.
Msimu uliopita, jezi hiyo ilikuwa ikitumiwa na Maka Edward ambaye sasa anatumia jezi namba 42

Adhabu ya Banka aliyefungiwa miezi 14 inaelekea ukingoni sasa akiwa tayari ameruhusiwa kufanya mazoezi na kikosi cha Yanga.
Mashabiki wa Yanga wanasubiri kwa hamu kumuona kiungo huyo Mzanzibar aliyetua kutoka klabu ya Mtibwa Sugar mwanzoni mwa msimu kwa mkataba wa miaka mitatu
Ataanza rasmi kuichezea Yanga Februari 08, 2019.
ADVERTISE HERE