Matajiri wamepigwa huko...!

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Dec 2018
Matajiri wamepigwa huko...!

Licha ya msemaji wa Simba Haji Manara  kutamba kuwa wana kikosi kipana kinachoweza kucheza michezo miwili kwa wakati mmoja, mambo yamewaharibikia tena baada ya Simba kuchapwa mabao 3-2 na Mashujaa Fc ya kutoka mkoani Kigoma katika mchezo wa kombe la FA (ASFC) raundi ya tatu uliopigwa kwenye uwanja wa taifa.

Simba imeondoshwa kwenye michuano ya kombe la FA katika raundi ta tatu, kama ilivyokuwa msimu uliopita walipoondoshwa na Green Worriors.

Sasa Simba italazimika kutwaa taji la ligi kuu ili iweze kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao. Swali ni kwamba Papaa Mwinyi Zahera anayeongoza ligi dhidi yao kwa tofauti ya alama 17 atakubali hilo jambo litokee? Kuna kila dalili hawatapanda ndege msimu ujao!

Matokeo ya mchezo mwingine uliopigwa leo, Mtibwa Sugar imeilaza Kiluvya United kwa mabao 3-0

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’