Boban arejea kikosini Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Dec 2018
Boban arejea kikosini Yanga

Kiungo Haruna Moshi 'Boban' anaweza kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoivaa Mbeya City Jumamosi ijayo, Disemba 29 katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kupona majeraha yake.

Juzi Boban aliichezea Yanga kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Tukuyu Stars na kupata majeraha (mshtuko wa nyonga) yaliyopelekea atolewe nje katika dakika ya 28.

Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amethibitisha kuwa hali ya mchezaji huyo inaendelea vizuri ambapo jana alifanya mazoezi mepesi ya kukimbia na leo anatarajiwa kuungana na wenzie katika maandalizi ya mchezo dhidi ya Mbeya City.

Kocha Mwinyi Zahera alitambia usajili wa kiungo huyo mkongwe akiahidi kuwa Boban atawanyamazisha wale wote wanaosema amekwisha.

Yanga inatarajiwa kuondoka kesho Alhamisi kuelekea mkoani Mbeya kwa usafiri wa ndege tayari kwa mchezo dhidi ya Mbeya City.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’