Sapoti ya mashabiki yampagawisha Kindoki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Dec 2018
Sapoti ya mashabiki yampagawisha Kindoki

Mlinda lango wa Yanga raia wa DR Congo Klaus Kindoki ameanza kudhihirisha makali yake baada ya leo kuonyesha uwezo mkubwa kwenye mchezo dhidi ya Tukuyu Stars.

Mashabiki wa Yanga waliokuwa uwanjani leo walimfanya Kindoki 'atambe' zaidi wakimshangilia kwa nguvu kila alipookoa mashambulizi ya Tukuyu Stars.

Katika mchezo huo Kindoki alifanikiwa kuokoa takribani mashambulizi matatu ambayo kama usingekuwa umahiri wake pengine Tukuyu Stars ingeweza kufunga.

Uungwaji mkono alioonyeshwa na washabiki wa Yanga leo umemfurahisha mlinda lango huyo ambaye hakuanza vizuri maisha yake katika klabu ya Yanga.

Kindoki sasa anaonekana kujiamini na kwa kiasi kikubwa ameimarisha kiwango chake na kuondoa makosa mengi aliyokuwa akiyafanya awali.

Yanga leo ilimtumia Kindoki mbele ya Kabwili ambaye alikuwa benchi baada ya kupona majeraha ya nyonga aliyopata kwenye mchezo wa ligi dhidi ya African Lyon.

Wakati hatma ya Beno Kakolanya ikiwa mikononi mwa kocha Mwinyi Zahera, kwa sasa Yanga inawategemea Kabwili na Kindoki.

Kakolanya alikuwepo uwanja wa Taifa leo kushuhudia mchezo huo ambayo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 4-0

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’