Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji ya TFF imemruhusu kiungo Haruna Moshi 'Boban' kuitumikia timu yake mpya ya Yanga aliyotua hivi karibuni akitokea klabu ya African Lyon.
Ruhusa hiyo inawahusu wachezaji wengine waliosajiliwa wakati wa dirisha dogo la usajili lililofungwa Disemba 15 2018.
Boban alishindwa kuitumikia Yanga kwenye michezo miwili ya ligi dhidi ya Ruvu Shooting na African Lyon akisubiri maamuzi hayo ya Kamati
Kesho Yanga itashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Tukuyu Stars katika mchezo wa kombe la FA (ASFC) raundi ya tatu.
Boban ameongeza idadi ya wachezaji wa Yanga ambao wanaweza kutumiwa na kocha Msaidizi Noel Mwandila kwenye mchezo huo
ADVERTISE HERE