Kiungo mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi ameanza mazoezi mepesi ya kukimbia ikiwa ni hatua kuelekea kurejea dimbani.
Mahadhi alipata majeraha mwezi August 2018 ambayo yamemuweka nje mpaka sasa. Alifanyiwa upasuaji wa goti mara mbili
Majeraha hayo ni kama yamemrudisha nyuma kiungo huyo aliyekuwa ameimarisha kiwango chake na kuweza kumshawishi kocha Mwinyi Zahera aliyemtumia katika michezo ya kombe la Shirikisho hatua ya makundi.
Kupona kwake kutazidi kukiimarisha kikosi cha Yanga ambacho pia kitaanza rasmi kupata huduma ya kiungo wake mpya Mohammed Issa 'Banka' aliyeruhusiwa kuanza mazoezi.
Banka ataanza rasmi kuitumikia Yanga Februari 08 2019.
ADVERTISE HERE