Zahera awapongeza wachezaji wake kwa ushindi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Dec 2018
Zahera awapongeza wachezaji wake kwa ushindi
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewapongeza wachezaji wake kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya African Lyon jana.

Zahera ambaye yuko nchini Ufaransa akishughulikia masuala yake binafsi ya kibiashara, amesema amefurahishwa na viwango vilivyoonyeshwa na vijana wake katika mchezo huo.

"Nimeambiwa Jaffar aliumia akaingia Kaseke akacheza vizuri sana. Rama nae akaumia na Kindoki akaingia pia akafanya vizuri",amesema

Hata hivyo Zahera amesikitishwa na kuumia kwa mlinda lango Ramadhani Kabwili na kiungo Jaffar Mohammed ambao walishindwa kumaliza dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Zahera amesema kuumia kwa wachezaji wake kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na ratiba isiyo rafiki ambapo amesema Yanga imecheza michezo saba ndani ya siku 20

"Wachezaji wetu wanaumia sana kwa kuwa wanacheza michezo mingi. Tumecheza michezo saba katika kipindi cha siku 18 siku 20 hilo limekuwa tatizo kwetu," amesema

Zahera anatarajiwa kurejea nchini Jumatano ijayo kuendelea na majukumu ya kuwanoa vinara hao wa ligi kuu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’