FT : African Lyon 0-1 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Dec 2018
FT : African Lyon 0-1 Yanga
Mabingwa wa kihistoria Tanzania, Yanga wameendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa African Lyon bao 1-0 katika mchezo uliopigwa dimba la Sheikh AMri Abeid mkoani Arusha.

Bao pekee la Yanga lilipatikana kwenye dakika ya 64 likiwekwa kimiani na beki 'mbishi' Abdallah Shaibu 'Ninja' aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na Ibrahim Ajib 'Miguu ya dhahabu'

Hilo lilikuwa bao la pili kwa Shaibu msimu huu huku Ajib akiendelea kujiongezea 'assists' sasa zikifika 12

Licha ya kukabiliwa na changamoto ya uwanja, Yanga ilicheza vizuri hasa katika kipindi cha pili.

Mabingwa hao wa kihistoria walipata pigo katika mchezo huo baada ya kuwapoteza wachezaji wake wawili kutokana na majeruhi.

Jaffard Mohammed alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia katika dakika ya 14 na nafasi yake kuchukuliwa na Deus Kaseke.

Mlinda lango tegemeo Ramadhani Kabwili nae aliumia nyonga na kushindwa kuendelea na mchezo katika dakika ya 38 na nafasi yake kuchukuliwa na Klaus Kindoki

Kabwili alikimbizwa Hospitalini kupatiwa matibabu zaidi

Ushindi huo umeikita Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama saba baada ya kufikisha alama 47
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’