Uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi katika klabu ya Yanga utafanyika Januari 13, 2019 kama ulivyopangwa.
Juzi Serikali kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe, iliweka msisitizo kuhusu kufanyika kwa uchaguzi huo baada ya kikao cha pamoja kati yake na viongozi wa TFF na Yanga.
Katika kuhakikisha uchaguzi huo hauvurugwi, Serikali imetangaza majina ya watu nane ambao wanatuhumiwa kushiriki mipango ya kuukwamisha uchaguzi huo.
Serikali imeyafikisha majina hayo katika vyombo vya usalama ili waweze kushughulikiwa.
Majina yaliyotajwa ni pamoja na Bakili Makele Mwenyekiti wa Matawi ya klabu ya Yanga ambaye tayari amefungiwa na TFF kujihusisha na soka.
Wengine ni Mustafa Mohamed, Edwin Kaisi, Said Bakari Lunguno, Shaban Mgonja, Kitwana Kondo, Boaz Ikupilika na David Sanare

ADVERTISE HERE