Yanga itaendelea 'kukimbiza' ikiwa na wachezaji hawahawa

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
19 Dec 2018
Yanga itaendelea 'kukimbiza' ikiwa na wachezaji hawahawa
Yanga haikufanya usajili wa maana katika dirisha dogo la lililofungwa wiki iliyopita na kuacha malalamiko mengi kwa viongozi wa timu hiyo.

Kiungo Haruna Moshi 'Boban' ndio mchezaji pekee ambaye alipendekezwa na Kocha Mwinyi Zahera aliyefanikiwa kusajiliwa.

Zahera aliutupia lawama uongozi wa Yanga kwa kushindwa kukamilisha usajili wa wachezaji wengine wanne huku akikerwa na kitendo cha uongozi wa timu hiyo kumdanganya kuwa usajili wa wachezaji hao ungekamilika

Lakini Mcongomani huyo amesema atatumia wachezaji waliopo ingawa hawezi kutoa ahadi ya kutwaa ubingwa.

Hata hivyo kushindwa kwa usajili wa wachezaji wapya kunaweza kuwa chachu ya kuwafanya wachezaji waliopo waongeze bidii zaidi ili kumshawishi kocha juu ya uwezo wao.

Ujio wa wachezaji wapya pengine ungeweza kuwaondoa baadhi ya wachezaji kikosini lakini sasa watakuwa na nafasi nyingine ya kumshawishi Zahera

Wachezaji hawa waliopo katika kikosi cha Yanga hawapaswi kukatishwa tamaa kwa kuhofia kuwa timu haitafanya vizuri eti kwa kuwa usajili uliopendekezwa haukufanikiwa

Hakuna ubishi kama wachezaji waliotakiwa na Zahera wangesajiliwa, Yanga ingekuwa moto zaidi lakini hata sasa ikiwa na hawa wachezaji waliopo Yanga haikamatiki

Wachezaji waliopo wameiwezesha Yanga kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi wakiongoza kwa tofauti ya alama nne dhidi ya Azam FC na alama 17 dhidi ya Simba inayojinasibu kuwa na kikosi cha zaidi ya Bil 1

Kama ilivyowashangaza wale ambao mwanzoni mwa msimu walikuwa wakiamini na wengine kudiriki kusema 'Msimu huu Yanga inapigania isishuke daraja', basi mwishoni mwa msimu pia Yanga itawashangaza wale wanaoamini kushindikana kwa usajili wa wachezaji wapya kutaigharimu timu hiyo.

Kitu pekee kinachoweza kuigharimu Yanga sasa ni labda akiondoka kocha Mwinyi Zahera ambaye amekuwa akifanya kazi ya ziada kuhakikisha timu inafanya vizuri.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
13h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
17h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
18h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
18h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’