Baada ya kuwasili mkoani Arusha leo, jioni kikosi cha Yanga kimefanya mazoezi kwenye viwanja vya Aghakhan kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya African Lyon utakaopigwa keshokutwa.
Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema wachezaji wote waliosafiri na timu hiyo wako katika hali nzuri kuelekea mchezo huo.
Amewataja Andrew Vicent na Raphael Daudi kuwa hawakusafiri na kikosi cha Yanga kutokana kuwa majeruhi.
Feisal Salum yeye ana kadi tatu za njano wakati Mrisho Ngasa anaendelea kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.
Papi Tshishimbi amepewa ruhusa ya kurejea kwao DR Congo kuhudhuria msiba wa Baba Mkwe wake.
Hafidh amesema kesho Yanga itafanya mazoezi kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid utakaotumika keshokutwa kwenye mchezo dhidi ya African Lyon.

ADVERTISE HERE