Kikosi cha mabingwa kihistoria wa Tanzania, Yanga kiko njiani kuelekea mkoani Arusha kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya African Lyon.
Mchezo huo utapigwa keshokutwa Alhamisi Disemba 20 katika dimba la Sheikh Amri Abeid.
Yanga imekuwa na msimu mzuri mpaka sasa ikiwa imeshuka dimbani mara 16, ikishinda michezo 14 na kutoka sare michezo miwili.
Iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 44, ikisalia na michezo mitatu kukamilisha duru ya kwanza ya michezo ya ligi kuu ya Tanzania Bara.

Vijana hao wa kocha Mwinyi Zahera wamepania kumaliza michezo yote ya duru ya kwanza bila ya kupoteza.
Baada ya kucheza na African Lyon, Yanga itakuwa na michezo miwili ya ugenini dhidi ya Mbeya City na Azam Fc

ADVERTISE HERE