Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuwa atarejea nchini Disemba 26 asubuhi baada ya kumaliza majukumu yanayompeleka nchini Ufaransa.
Aidha Zahera amebainisha kuwa kilichompeleka Ufaransa sio ugonjwa bali ni masuala ya biashara zake ambapo kuna 'document' ametakiwa kwenda kusaini.
"Jamani mimi nipo nakwenda Ufaransa mara moja na nitarudia tarehe 26 asubuhi. Nakwenda huko kuna makaratasi nimetakiwa kusaini," amesema Zahera katika video fupi iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii
Tangu kuibuliwa kwa taarifa kuhusu kusafiri kwa Zahera mapema leo asubuhi, kumekuwa na wasiwasi miongoni mwa mashabiki wa Yanga kuwa huenda kocha huyo ameondoka moja kwa moja.
"Mimi nimekuwa mstari wa mbele kuwahamasisha wachezaji wavumile hali ngumu iliyo klabuni kwa sasa halafu mimi ndio nikimbie? haiwezekani," alisema

ADVERTISE HERE