Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewakutanisha viongozi wa TFF na klabu ya Yanga kusaka suluhu juu ya mvutano baina ya pande hizo kuhusu uchaguzi wa Yanga uliopangwa kufanyika Januari 13 2019.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Jaji John Mkwawa, Hussein Nyika, Siza Lyimo, Thobias Lingalangala na Samwel Lukumay kwa upande wa Yanga, wakati upande wa TFF waliwakilishwa na rais Wallace Karia, Makamu wa rais, Athuman Nyamlani, na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa TFF, Ally Mchungahela
Uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi katika klabu ya Yanga umegubikwa na sintofahamu baada ya viongozi wa Yanga kupinga mchakato huo kusimamiwa na TFF
Nao TFF wamesisitiza kuwa na mamlaka yote ya kuendesha uchaguzi hali iliyopelekea wanachama wa Yanga kutishia kwenda Mahakamani kuzuia mchakato huo mpaka pale Mahakama itakapoamua juu mwenye haki ya kuendesha mchakato wa uchaguzi wa Yanga.
Dk Mwakyembe ameahidi kuupatia suluhu mgogoro huo ili uchaguzo ufanyike kwa amani kama ulivyopangwa

ADVERTISE HERE