Ukiwauliza viongozi wa Yanga leo kwa nini mambo mengi hayafanikiwi kunako klabu hiyo watakwambia ni kwa sababu ya kukosekana kwa fedha.
Lakini inashangaza kuona viongozi hao wamekosa ubunifu wa kutumia mtaji mkubwa wa mashabiki walionao kuongeza kipato cha timu hiyo.
Yanga inaaminika kuwa na takribani mashabiki wanaoweza kufika Mil 20 na ndio timu yenye mashabiki wengi zaidi hapa Tanzania
Viongozi wa Yanga wanaona njia pekee ya kuongeza mapato ya timu ni kupitisha bakuli tu, utaratibu ambao kwanza sio endelevu lakini pia 'unakera' na unaidhalilisha timu.
Hatukatai utaratibu huo upo kwa timu zote duniani lakini sio utaratibu rasmi. Siku zote mashabiki na wanachama wanajitoa kwa ajili ya timu zao kwa utashi wao.
Viongozi wa Yanga ilipaswa wabuni miradi ambayo itaweza kuiongezea timu mapato. Kwani tayari wana wateja karibu Mil 20 mezani
Kwa mfano, kama Yanga itakuja na bidhaa ambayo itauzwa kwa Shilingi elfu moja na kila mwezi ikanunuliwa na wateja Milioni moja (Kati ya Mil 20 waliopo) timu itaingiza Bil moja kila mwezi.
Yaweza isifike kiwango hicho lakini hoja ya msingi hapa ni kuwa timu itakuwa inaweza kujitegemea kwa kujiingizia kipato chake na kuweza kumudu gharama za uendeshaji
Haya, tangu mwanzoni wa msimu mashabiki wa Yanga wamekuwa wakiuliza wapi watapata jezi halisi za timu hiyo. Lakini mpaka leo duru ya kwanza ya ligi inaelekea ukingoni hakuna majibu.
Kila siku viongozi wanatambulisha jezi mpya lakini haijulikani zinapatikana wapi? (Hakuna sehemu rasmi ya timu zaidi ya watu binafsi wanaouza jezi feki)
Wakati fulani kuna mdau alihoji uongozi wa Yanga umeshindwa hata kuwa na duka lake la kuuza vifaa pale Makao Mkuu ya klabu?
Kwamba hata kama mmeshindwa kuweka utaratibu wa kusambaza mikoani bado mmeshindwa hata kuweka duka hapo Dar ili kila mwenye kuweza akaja kununua mwenyewe?
Leo hii Yanga inafanya vizuri lakini hali yake ni mbaya sana. Inahitaji mabadiliko ya haraka ya uongozi ili kuweza kuinusuru na anguko kubwa linaloinyemelea.
Kocha Mwinyi Zahera amewasaidia mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kufahamu nini kinachoendelea ndani ya timu yao.
Zahera ameonyesha kuwa na upendo na WanaYanga kutokana na ukarimu wao kwake hivyo nae amejitoa kujaribu kuinusuru timu hiyo ambayo furaha iliyopo inaweza kutoweka wakati wowote kama hatua za haraka hazitachukuliwa.
Januari 13 2019 kutakuwa na uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi. Ni vyema Wanachama wa klabu hiyo wakaacha kupinga uchaguzi badala yake wajikite kwenye hoja ya kuhakikisha unafanyika kwa misingi ya Yanga.
Lakini kwa hali ilivyo ni dhahiri Yanga inahitaji watu wapya, watakaokuja na mawazo mapya na akili za kibiashara kuiondoa timu kwenye dimbwi la umasikini wa kujitakia

ADVERTISE HERE