Nini kilikwamisha usajili wa wachezaji wanne Yanga?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Dec 2018
Nini kilikwamisha usajili wa wachezaji wanne Yanga?
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amefichua kuwa jana alikaribia kuachana na timu hiyo na kurejea kwao baada ya kutofurahishwa na 'madudu' yaliyofanywa na viongozi wa timu hiyo kwa kushindwa kukamilisha usajili wa wachezaji aliowaagiza.

Zahera amesema amebaki Yanga kwa sababu ya mashabiki wa timu hiyo

Zahera amebainisha kuwa siku mbili kabla ya dirisha la usajili kufungwa, viongozi wa timu hiyo walimtaarifu kuwa walikuwa katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa mlinda lango Farouq Shikalo kutoka Bandari Fc ya Kenya, washambuliaji Charles Ilanfya (Mwadui Fc) na Umar Kasumba (Sofapaka Kenya) huku viongozi hao pia wakishindwa kumsajili Reuben Bomba kwa mkataba wa muda mfupi.

Amesema hadi masaa mawili kabla ya dirisha la usajili kufungwa alikuwa na matumaini kuwa usajili wa wachezaji hao tayari umekamilika

Hata hivyo alitaarifiwa kuwa wameshindwa kuwasajili muda mchache kabla ya dirisha la usajili kufungwa kitendo kilichomuumiza sana.

Zahera ameongeza kuwa viongozi wa Yanga wamemuharibia mipango yake na amewaambia wasije wakamuuliza kulikoni kama timu itashindwa kufanya vizuri

Zahera amebanisha kuwa alipanga kuimarisha kikosi chake ili kwenye duru ya pili ya ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga iweze kuwa washindani halisi katika mbio za ubingwa.

Zahera aliyeonekana kukerwa na tukio hilo amesema anajitoa sana kuifundisha Yanga na kayuko hapo kwa ajili ya fedha

Swali la kujiuliza ni nini kilichopelekea usajili wa wachezaji hao ukashindwa kukamilika?

Huenda viongozi wa Yanga hasa Mwenyekiti wa Kamati ya usajili atakuwa na majibu sahihi
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’