Wachezaji wa Yanga wameendelea kudhihirisha kuwa msimu huu wanautaka kwelikweli ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara.
Bila ya kujali changamoto zinazowakabili, wachezaji wameendelea kuipigania timu kuhakikisha inapata matokeo.
Mchezo wa leo dhidi ya Ruvu Shooting haukuwa mwepesi na ushindi uliopatikana ni matokeo ya kujituma kwa vijana wa kocha Mwinyi Zahera.
Upambanaji huu pia ulionyeshwa kwenye michezo dhidi ya Prisons na Biashara United ambapo Yanga ililazimika kutokea nyuma na kupata ushindi.
Zahera amefanikiwa kuwajenga wachezaji wake kisaikolojia kiasi kwamba hawako tayari kupoteza mchezo, akili yote iko katika kushinda.
Kwa wanaosubiri Yanga ifungwe ili wapate 'ahueni' huenda wakasubiri mpaka mwishoni mwa msimu na jambo hilo linaweza lisitokee.

ADVERTISE HERE