Ligi kuu bara kuanza Jumamosi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Aug 2017
Ligi kuu bara kuanza Jumamosi
Michezo ya ufunguzi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayozihusisha timu za Dar es Salaam itachezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, maarufu kama Shamba la Bibi kutokana na Uwanja wa Taifa kuingia kwenye programu ya upandikizaji upya wa nyasi.

Msimu mpya wa Ligi Kuu wa 2017/2018 unaanza rasmi Jumamosi y Agosti 26, 2017 kwa michezo saba itayochezwa katika viwanja tofauti nchini kutafuta bingwa atakayeshiriki pia Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2019.

Kwa mechi za kesho Jumamosi, Simba inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakati Mbao watakuwa wageni wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Majimaji ya Songea itakayosafiri hadi Mbeya kucheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini humo huku Njombe Mji ikiialika Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Sabasaba huko Makambako.

Kadhalika Uwanja wa Manungu ulioko Turiani, Mtibwa mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar itaikaribisha Stand United ya Shinyanga kwenye mchezo mwingine wa VPL ilihali Azam atakuwa mgeni wa Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Mwadui watakuwa wenyeji wa Singida United ya Singida kwenye Uwanja wa Mwadui huko Shinyanga na Jumapili kutakuwa na Mchezo mmoja utakaowakutanisha mabingwa watetezi, Yanga SC dhidi ya Lipuli ya Iringa Uwanja wa Uhuru.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’