Ibrahim Hamid na Haruna Moshi 'Boban' ndio wachezaji pekee walioongezwa kwenye kikosi cha Yanga katika dirisha dogo la usajili lililofungwa usiku wa kuamkia leo.
Wakati Boban akiwa anafahamika na wengi, Hamid ni mgeni miongoni mwa mashabiki wa soka nchini.
Hamid ni mlinda lango ambaye wakati flani aliwahi kuitumikia Ashanti United ya jijini Dar es salaam.
Yanga inapita katika kipindi kigumu cha kiuchumi, ni lazima mashabiki wafahamu kwani hakuna muujiza ambao ungeweza kutokea kwenye usajili huu wa dirisha dogo.
Hamid amefanya majaribio Yanga na uwezo wake umemridhisha kocha Mwinyi Zahera na benchi lake la ufundi.
Kwa mazingira inayopita Yanga hasa baada ya sintofahamu iliyomkumba aliyekuwa mlinda lango wake namba moja Beno Kakolanya, ilikuwa ni lazima kusaka mlinda lango mwingine haraka.
Sasa kuhusu uwezo wake ni vyema mashabiki wakawa na subira kuliko kuanza kuponda wakati bado hajaonekana dimbani, uzuri mchezo wa soka unachezwa hadharani.

ADVERTISE HERE