Usajili wa Boban 'wamkosha' Yondani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
16 Dec 2018
Usajili wa Boban 'wamkosha' Yondani
Nahodha wa Yanga Kelvin Yondani amezungumzia usajili wa mkongwe Haruna Moshi 'Boban' kuwa utainufaisha timu hiyo.

Yondani anayefahamiana vizuri na Boban ambaye walicheza pamoja timu ya Simba, amesema baada ya kuwa na kikosi kilichosheheni wachezaji wengi vijana, ilikuwa ni muhimu kwa Yanga kuongeza wachezaji wakongwe kama Boban ambao wana uzoefu utakaosaidia kuipa timu mafanikio.

Yondani amewataka mashabiki wa Yanga kuwa na subira kuona 'vitu' vya Boban dimbani huku akiwaambia wale wanaokosoa kuwa watatulia atakapoanza kuitumikia timu hiyo

“Kama unakumbuka msimu uliopita timu yetu ilikuwa ina watoto wengi hali iliyosababisha tuukose ubingwa kutokana na kukosa uzoefu wakati timu ikipambana kupata matokeo mazuri," Yondani amenukuliwa na hazeti la Championi

“Niliwahi kuwashauri viongozi tusajili wachezaji wakongwe kama akina Boban wenye uzoefu na watakaobadilisha matokeo ndani ya uwanja, hivyo nashukuru wamelifanyia kazi.

“Utaona walianza kumsajili Ngasa leo hii utaona mchango mkubwa anautoa katika timu kuzidi hao vijana aliowakuta, wanastahili pongezi katika hilo."

Yondani alifichua usajili wa Boban kutua Yanga mapema wakati uongozi wa Yanga ukiwa bado haujaweka wazi kuhusu usajili huo.

Yondani na Boban ni wachezaji marafiki wanaofahamiana vizuri kwa zaidi ya miaka kumi.

Kwenye mtandao wa Instagram, Boban anapatikana kwa jina la boban3_officialtz
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →