Kikosi cha Yanga leo Jumapili kinatarajiwa kushuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara mzunguuko wa 17.
Yanga itakuwa na nafasi ya kujiimarisha kileleni kwa tofauti ya alama nne kama itashinda mchezo huo.
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema anatarajia mchezo huo utakuwa mgumu zaidi ya michezo waliyocheza dhidi ya Prisons na Biashara United.
Yanga itawakosa baadhi ya wachezaji wake kama Kelvin Yondani, Mrisho Ngasa, Thabani Kamusoko na Raphael Daudi kutokana na sababu za majeruhi na adhabu za kadi
Hata hivyo Zahera amesema hana wasiwasi na kukosekana kwa wachezaji hao kwani anao wachezaji wa kucheza katika nafasi zao
Ibrahim Ajib aliyekosa mchezo dhidi ya Biashara United atarejea kikosini leo baada ya kumaliza adhabu.
Mchezo utapigwa kuanzia saa kumi jioni ambapo viingilio ni VIP A Tsh 15,000/-, VIP B na C Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-

ADVERTISE HERE