Usajili wa Boban tuweke akiba ya maneno

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
14 Dec 2018
Usajili wa Boban tuweke akiba ya maneno
Tangu kuondoka kwa Yusufu Manji, Yanga imekuwa haifanyi 'makeke' makubwa kwenye usajili wake, kuyumba kwa uchumi ikitajwa kuwa sababu.

Mwanzoni mwa msimu Yanga ilisajili wachezaji saba ambao hawakuwa na majina makubwa.

Miongoni mwao alikuwepo mkongwe Mrisho Ngasa ambaye usajili wake ulipingwa vikali na baadhi ya mashabiki.

Lakini baada ya kuitumikia Yanga kwa takribani michezo 14, imedhihirika ulikuwa uamuzi sahihi kwa viongozi wa timu hiyo kumrejesha Ngasa aliyejijengea heshima ya kipekee kunako mitaa ya Jangwani.

Ngasa mwenye umri wa miaka 29 ni miongoni mwa wachezaji wanaofanya vizuri kwenye ligi msimu huu akiwa amefunga mabao manne.

Jana Yanga imethibitisha kumsajili mkongwe Haruna Moshi Shaban 'Boban' ambaye mwezi Mei mwaka huu alitimiza miaka 31.

Usajili wake lilikuwa hitaji la kocha Mwinyi Zahera ambaye amemsifia kiungo huyo kuwa ana uwezo mkubwa.

Boban ametua Yanga akiwa tayari ameifungia Lyon mabao mawili msimu huu.

Kwa wale waliomfuatilia Boban katika kikosi cha African Lyon hawawezi kuhoji juu ya usajili wake kwani ameonyesha bado mguu wake una 'madini'

Boban atawashangaza wengi kama ilivyokuwa kwa Ngasa.

Mara nyingi Zahera amekuwa akisisitiza kuwa mshambuliaji wake Heritier Makambo licha kufunga mabao nane mpaka sasa, bado hajafikia kiwango chake kwa kuwa hajapata mtu sahihi wa kumrahisishia kazi pale mbele

Boban amedhihirisha kuwa na uwezo wa kucheza nafasi ya mshambuliaji msaidizi na kutengeneza nafasi za mabao.

Bila shaka Zahera amemuongeza katika kikosi cha Yanga kwa ajili ya kazi hiyo

Mkongwe huyo ataongeza ubunifu katika kikosi cha Yanga na sijui itakuwaje watakapokutana na fundi Ibrahim Ajib ambaye tayari mguu wake umehusika katika mabao 15 ya Yanga

Ni vyema mashabiki wakaweka akiba ya maneno kuhusu usajili wake kwani tukumbue; kwa ligi ya hapa kwetu imedhihirika wakongwe ndio wanaofanya vizuri zaidi kuliko wachezaji chipukizi

Lakini pia jambo la msingi zaidi ni kuwa Yanga tayari inafanya vizuri ikiwa na kikosi hiki hiki kinaonekana kama cha 'kuungaunga'.

Kocha Mwinyi Zahera amekuwa akifanya maamuzi sahihi ya kuchagua aina ya wachezaji anaowatumia kulingana na michezo na ameisaidia Yanga mpaka sasa kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi.

Anafahamu kitu anachokihitaji kutoka kwa Boban.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
4h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’