Uongozi wa klabu ya Yanga umesema bado unamsubiri mlinda lango wake Beno Kakolanya aripoti mazoezini kabla ya kumchukulia hatua zaidi.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Hussein Nyika ambaye ndiye anayeongoza Kamati ya usajili amesema Yanga haijachukua hatua yoyote dhidi ya mlinda lango huyo mpaka sasa.
Lakini inamsubiri aripoti kambini ili atoe maelezo ya nini kilichomfanya atoweke klabuni kwa zaidi ya mwezi mzima
"Sisi kama viongozi tunamsubiri Beno arudi mazoezini tumuulize alikuwa wapi. Hatuwezi kufanya kazi ya kumtafuta mchezaji," amesema Nyika
Kakolanya anadaiwa kuuandikia barua uongozi wa Yanga akiomba kuvunja mkataba wake akidai kutomaliziwa fedha zake za usajili na kutolipwa mishahara ya miezi kadhaa.
Mlinda lango huyo amekuwa akihusishwa kutaka kuelekea kunako klabu ya Simba.

ADVERTISE HERE