Wakati dirisha dogo la usajili likitarajiwa kufungwa ndani ya saa 48, mabosi wa Yanga wako kimya ikielezwa watalipua 'mabomu' wakati wowote
TFF imetoa mwongozo kuhusu usajili huo wa dirisha dogo uliofunguliwa Novemba 15 na utafungwa keshokutwa Jumamosi, Disemba 15
Hakutakuwa na muda zaidi utakao-ongezwa baada ya dirisha hilo kufungwa.
Juzi Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika alisema mabingwa hao wa kihistoria wako mbioni kukamilisha usajili wa wachezaji wanne, ambapo wawili wanatoka nje ya nchi na wawili ni kutoka humu nchini.
Hata hivyo mpaka sasa bado ni tetesi tu zinazozungumzwa zaidi kuhusu usajili wa Yanga huku Nyika akigoma kuweka wazi ni wachezaji gani ambao tayari wamesaini mikataba.
Yanayoripotiwa na vyombo vya habari
Mkongwe Haruna Moshi 'Boban' jina lake limetawala vyombo vya habari ikielezwa tayari amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga
Nyika aligoma kuweka wazi kuhusu usajili wa mchezaji huyo wa African Lyon akitaka wadau wasubiri hadi dirisha la usajili litakapofungwa kufahamu ukweli.
Uongozi wa Yanga pia unaelezwa kuwa katika mchakato wa kusaka mlinda lango mbadala wa Beno Kakolanya ambaye yuko katika mgomo akishinikiza alipwe malimbikizo ya mishahara na fedha za usajili ambazo hakulipwa
Mlinda lango wa Tanzania Prisons Aaron Kalambo amehusishwa kutaka kusajiliwa na Yanga kabla dirisha la usajili kufungwa.
Pia Yanga inaelezwa kuwa imewasiliana na klabu ya Bandari FC ya Kenya ikitaka kumsajili mlinda lango wa timu hiyo Farouq Shikalo ambaye pia ni mlinda lango namba moja wa timu ya Taifa ya Kenya
Miongoni mwa wachezaji kutoka nje wanaodaiwa kuwa mbioni kutua Yanga ni mshambuliaji wa Sofapaka, Mganda Umar Kasumba
Inaelezwa tayari Yanga imemalizana na mshambuliaji huyo aliyekuwa akisubiriwa kusaini mkataba tu
Zahera hajaridhishwa na Bomba
Inaelezwa winga Reuben Bomba aliyeletwa nchini baada ya kupendekezwa na kocha Mwinyi Zahera huenda asisajiliwe baada ya Zahera kubaini kiwango chake kimeshuka
Bomba anayejifua na kikosi cha Yanga tangu mwanzoni mwa wiki hii, hakuwa amesaini mkataba licha ya makubaliano ya awali kufikiwa
Huenda Yanga ikasajili mchezaji mwingine wa ndani ambapo mshambuliaji wa Mwadui Fc Charles Ilanfya anatajwa kuwa moja ya mapendekezo ya Zahera.

ADVERTISE HERE