Kukaa nje hakumsaidii Beno ajitafakari - Ivo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
13 Dec 2018
Kukaa nje hakumsaidii Beno ajitafakari - Ivo
Mlinda lango mkongwe Ivo Mapunda amemshauri kipa wa Yanga Beno Kakolanya kutafakari upya uamuzi wake wa kugoma akishinikiza alipwe madeni anayoidai Yanga

Ivo aliyewahi kun'gara hapa Tanzania, Kenya na Ethiopia amesema mgomo huo anaofanya unam-maliza yeye mwenyewe.

Kuendelea kukaa nje bila kucheza kwa muda mrefu kutashusha kiwango chake pia kutaondoa imani kwa kocha wake Mwinyi Zahera na hata akiondoka Yanga rekodi hiyo itaendelea kumfuata huko aendako

“Kakolanya ni kipa mzuri, ila anachokifanya sasa ni kujidanganya maana kiwango chake kinashuka, kukaa nje muda mrefu hakumjengi mchezaji hata kama hana mpango wa kucheza Yanga huko anakokwenda anapoteza uaminifu labda kama anaenda nje pia wanafuatilia hadi mechi ya mwisho pamoja na historia ya mchezaji," Ivo amenukuliwa na Mwanaspoti

“Miaka michache iliyopita tulikuwa tunaangalia zaidi kupata nafasi ya kucheza ili uonekane na timu zingine, masilahi lilikuwa jambo la pili ila sasa ni tofauti kabisa na wachezaji wetu hawa, masilahi kwanza kucheza baadaye bila kujali wanapeleka wapi viwango vyao, hii inawaumiza wachezaji wengi.

“Kakolanya ni kijana mwenye umri mdogo kukaa nje kunamuumiza yeye na si mtu mwingine, Yanga sasa hivi inafanya vizuri angekuwepo yeye nafasi yake ilikuwa wazi sana ya kucheza lakini Ramadhan Kabwili kakamata dimba na ataendelea kuwa bora zaidi baada ya Klause Kindoki kutoka mchezoni alipofanya vibaya kwenye mechi za nyuma”

Kwa mwezi mmoja sasa Kakolanya amejiondoa kwenye kikosi cha Yanga akishinikiza alipwe pesa ya usajili iliyobaki na mishahara ya miezi kadhaa ambayo hajalipwa

Hata hivyo uongozi wa Yanga umesisitiza kuwa wachezaji wote wanaidai klabu hiyo na wamekuwa wakilipa madai hayo kwa awamu

Lakini ni Kakolanya pekee aliyeondoka kabisa kwenye kambi ya klabu hiyo huku Kocha Mwinyi Zahera akisema hafahamu alipo mchezaji huyo na hajamuona tangu aliporejea kutoka DR Congo kutimiza majukumu ya timu ya Taifa

Kakolanya aligoma kujiunga kwenye kikosi cha Yanga baada ya kurejea kutoka Lesotho na timu ya Taifa mwezi uliopita

Sintofahamu kuhusu mlinda lango huyo imeshika kasi zaidi baada ya kubainika wakala wake ni kiongozi mwandamizi katika klabu ya Simba.

Wengi wanauchukuliwa mgomo huo kama hujuma kwa Yanga ambayo ilikuwa ikimtegemea zaidi mlinda lango huyo baada ya Klaus Kindoki kuonyesha udhaifu mkubwa

Hata hivyo kinda Ramadhani Kabwili ameweza kuisaidia Yanga kushinda michezo yote mitano aliyodaka na hivyo kupunguza thamani ya Kakolanya kwenye kikosi cha Yanga.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
38m ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →