Yanga imepania kweli kweli msimu huu kuhakikisha inafanya vizuri kwenye michuano yote itakayoshiriki.
Baada ya ratiba ya raundi ya tatu ya michuano ya kombe la FA (ASFC) kutolewa, uongozi wa timu hiyo umesema hawatadharau timu watakayokutana nayo kwenye michuano hiyo
Vinara hao wa ligi kuu ya Tanzania Bara wamepangwa kuanzia jijini Dar es salaam dhidi ya mshindi wa mchezo kati ya Ihefu fc dhidi ya Tukuyu Stars zote kutoka jijini Mbeya
Timu hizo zitachuana mwishoni mwa wiki hii kumpata mshindi atakayeifuata Yanga jijini Dar es salaam kati ya Disemba 20-24
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema wanafanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha wanatinga raundi inayofuata kwenye michuano hiyo.
Ten amesema kwa uzoefu walioupata msimu uliopita, wanafahamu mchezo huo hautakuwa mwepesi na wanapaswa kujiandaa kikamilifu ili kuweza kupata matokeo
Msimu uliopita Yanga ilitolewa na Singida United kwa mikwaju ya penati kwenye hatua ya robo fainali.
Ilichuana na Ihefu Fc katika hatua ya 16 bora jijini Mbeya na kufanikiwa kutinga robo fainali kwa ushindi wa penati 4-3 baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1
Yanga ilisawazisha bao kwenye dakika za majeruhi kupitia kwa Obrey Chirwa ambaye sasa amejiunga na Azam Fc

ADVERTISE HERE