TFF yafafanua kuhusu tuhuma za ubadhilifu wa Mil 300

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Dec 2018
TFF yafafanua kuhusu tuhuma za ubadhilifu wa Mil 300
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linapenda kufafanua kuhusu taarifa katika baadhi ya vyombo vya Habari kuwa kumekuwa na ubadhirifu wa fedha ndani ya TFF.

Taarifa hiyo iliyochapwa kwenye gazeti la Tanzanite toleo namba 292 la Jumatatu Disemba 10,2018 lenye kichwa cha habari KASHFA TFF,ZAIDI YA 300M/- ZATAFUNWA.

Taarifa hiyo imejikita kwenye Taarifa ya Hesabu za TFF za mwaka 2015 na 2016 zilizopokelewa tarehe 11 Septemba 2016 na tarehe 27 Novemba 2017 kwa mfuatano na kufanyiwa kazi.

Katika kipindi hicho kilichotajwa kimekuwa chini ya ukaguzi wa PCCB na tayari mashauri yako mahakamani yanaendelea ikiwa ni pamoja na kufuatilia waliotajwa katika hesabu za fedha katika kipindi cha mwaka 2015 na 2016.

Kwa kuwa masuala hayo yapo kwenye ngazi ya mahakama, TFF inaona iviachie vyombo vya kisheria vifanye kazi yake kadiri ya taratibu zao.

Cliford Mario Ndimbo
Afisa Habari na Mawasiliano,TFF
Disemba 11,2018
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’