Ajib awapa neno wanaomfananisha na Chama

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Dec 2018
Ajib awapa neno wanaomfananisha na Chama
Siku chache zilizopita kumeibuliwa mjadala kwenye mitandao ya kijamii baada ya mdau mmoja wa soka kuchambua uwezo wa wachezaji Ibrahim Ajib wa Yanga na Cleotus Chama wa Simba na kufikia mwafaka kuwa Ajib ni bora zaidi ya Mzambia huyo kutokana na ukweli kwamba Ajib anan'gara akiwa kwenye kikosi kilicho na mazingira magumu.

Hata hivyo hilo lilipingwa vikali na Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara pamoja na mashabiki wengi wa Simba wanaodai kuwa Chama ndiye mchezaji bora zaidi wa sasa hapa nchini na huku Manara akienda mbali zaidi kwa kusema pengine Chama ndiye mchezaji bora zaidi kuwahi kucheza nchini.

Hata hivyo jana mashabiki wa Yanga walimkumbusha Manara kuwa baba yake mzazi, Sunday Manara alikuwa bora sana nyakati zake hadi kupachikwa jina la 'Computer'.

Hivyo kusema hajawahi kutokea mchezaji kama Chama hapa Tanzania ni kumkosea heshima baba yake mzazi ambaye amejijengea heshima ya kipekee katika klabu ya Yanga na nchi kwa ujumla.

Nae Ajib aliyelengwa kwenye mjadala huo ametia neno kuwa anafarijika kuona kila mchezaji anayedhaniwa ni bora basi ni lazima ashindanishwe nae

Ajib amesema jambo hilo litaendelea kutokea hata watakapowaleta wachezaji wengine.

Ukiachana na maneno ya mashabiki, takwimu zinambeba Ajib kuwa kiungo bora zaidi miongoni mwa wote wanaoshiriki ligi kuu ya Tanzania Bara msimu huu.

Ajib amefunga mabao matano na ametengeneza mabao 10. Kwa jumla amehusika kwenye mabao 15 kati ya 29 yaliyofungwa na Yanga mpaka sasa.

Chama anayeaminishwa kuwa bora sana, amefunga mabao mawili na kutengeneza mawili tu.

Ubora wa mchezaji haupimwi kwa chenga zake za maudhi au kuuchezea mpira bali utapimwa kutokana na mchango wake kwa timu husika.

Leo hii akina Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wametwaa tuzo nyingi za mwanasoka bora wa dunia kuliko wengine wote kutokana na mchango wao kwa timu zao.

Naamini wapo wachezaji wengi mafundi zaidi yao lakini kwa kuwa hawakuzisaidia timu zao kufanya vizuri waliishia kusifiwa tu bila ya kupata tuzo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’