Licha ya kuwa ulikuwa mchezo wake wa kwanza wa ushindani kwenye kikosi cha Yanga, Papi Kabamba Tshishimbi amedhihirisha hana mpinzani kwenye nafasi ya kiungo mkabaji (CDM).
Umahiri wake wa kukaba, kupokonya mipira, kuanzisha mashambulizi na kupiga pasi za uhakika kumemfanya apigiwe kura nyingi za kuwa nyota wa mchezo wa jana dhidi ya Simba.
Tshishimbi akishirikiana vyema na Kamusoko na Alpha waliwapa wakati mgumu viungo wa Simba waliokuwa wakiongozwa na Haruna Niyonzima washindwe kutamba
Kamati ya usajili iliyokuwa ikiongozwa na Hussein Nyika inastahili pongezi kwa kufanikisha kusajiliwa kwa kiungo huyu ambaye alikuwa akinyemelewa na Orlando Pirates ya Arika Kusini.
Kwa hakika Tshishimbi ameiimarisha Yanga kwenye ulinzi na sehemu ya kiungo. Uwepo wake pia unampa Uhuru Thabani Kamusoko kuweza kuchezesha timu.
Wale waliokuwa wanadhani kuondoka kwa Niyonzima kutaacha pengo Yanga sasa wamefahamu, Yanga imeimarika zaidi.

ADVERTISE HERE