Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema hafahamu alipo mlinda lango Beno Kakolanya
Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya mchezo dhidi ya Biashara United, Zahera alisema mlinda lango huyo ana mgogoro na uongozi wa Yanga.
Aidha Zahera ameshangaa baada ya kupewa taarifa kuwa wakala wa Kakolanya ni kiongozi wa klabu ya Simba.
"Walinitaarifu kuwa agent wa Beno ni kiongozi katika klabu ya Simba nikashangaa sana," alisema
Licha ya Yanga kukabiliwa na changamoto za kiuchumi, wachezaji wameendelea kutekeleza majukumu yao isipokuwa Kakolanya ambaye ameondoka kabisa klabuni.
Kumekuwa na taarifa kuwa Kakolanya anataka kuvunja mkataba wake na Yanga ili aweze kujiunga Simba akiwa mchezaji huru.

ADVERTISE HERE