Ishu ya Manji kumbe dawa za usingizi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Aug 2017
Ishu ya Manji kumbe dawa za usingizi
Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Domician Dominic, ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa dawa aina ya Benzodiazepines iliyokutwa katika sampuli ya mkojo wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusufali Manji, hutumika hospitalini kutuliza maumivu makali ama kumpatia mtu usingizi.

Shahidi huyo wa tatu wa upande wa mashtaka aliyaeleza hayo jana akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu,Timon Vitalis kutoa ushahidi katika kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin inayomkabili mfanyabiashara huyo. .

Akitoa ushahidi, Dominic alidai katika uchunguzi wa awali alioufanya katika sampuli ya mkojo wa Manji alikuta una dawa aina ya Benzodiazepines.

Alidai yeye kama Mkemia, kuwepo kwa dawa hiyo kwenye sampuli hiyo ya mkojo kulimpa picha kuwa mtu huyo alikuwa anaitumia kwa kutuliza maumivu makali au kukosa usingizi na kwamba ina matumizi mengi.

Pia alisema kwa uzoefu wake mara nyingi mtu anayetumia dawa hiyo huwa anatumia Heroine ama cocaine.

Manji aliyekana mashtaka anawakilishwa na Mawakili Alex Mgongolwa, Hudson Ndusyepo na Mosses Kimaro.

Kwa hisani ya Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’