Licha ya kuelezwa kuwa na hali ngumu ya kiuchumi, uongozi wa klabu ya Yanga umekuwa ukihakikisha wachezaji wa timu hiyo hawachoshwi na safari za mikoani kwa kusafiri na ndege.
Yanga imetumia usafiri wa Ndege kwenda Mwanza, Kagera na Mbeya kuzikabili Mwadui FC, Kagera Sugar na Tanzania Prisons katika michezo ya ligi kuu ya Tanzania Bara
Leo Yanga inarejea jijini Dar es salaam ikitokea mkoani Mbeya kwa usafiri huo huo.

Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema usafiri wa ndege unawasaidia kupunguza uchovu wa wachezaji ambao ungepatikana kama wangetumia basi
Saleh amesema usafiri huo kwa kiasi kikubwa umewasaidia wachezaji wao kuwa katika hali nzuri kimchezo

ADVERTISE HERE