Ni dhahiri kwa sasa uongozi wa Yanga hauna namna yoyote ya kukwepa uchaguzi wa kupata viongozi wapya ikiwemo nafasi ya Mwenyekiti kutokana na kuwepo uwezekano mdogo wa aliyekuwa Mwenyekiti wake Yusufu Manji kurejea katika nafasi yake.
Licha ya kuwa na mapenzi makubwa kwa klabu ya Yanga, wakati huu Manji amekuwa akikabiliwa na changamoto lukuki zinazotishia hata ustawi wa biashara zake
Bilionea huyo huenda akahitaji muda zaidi wa kushughulikia changamoto hizo kuliko inavyofikiriwa.
Leo gazeti la Mwananchi limeripoti kuwa mali za mfanyabiashara huyo zenye thamani ya mabilioni ya shilingi ziko hatarini kufilisiwa baada ya kuwekwa chini ya wadhibiti na wakabidhi wasii ili kulipa madeni makubwa yanayodaiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki na Kusini.
Mali hizo ni pamoja na jengo maarufu jijini Dar es Salaam lijulikanalo kwa jina la Quality Centre.
Taarifa zilizotolewa jana na wafisili na wakabidhi wasii hao chini ya Kampuni ya Price Water House Coopers (PWC), ilisema kuanzia jana, Manji hataruhusiwa kumiliki mali hizo hadi atakapolipa madeni hayo.
Tayari Serikali imeushauri uongozi wa Yanga kukamilisha mchakato wa uchaguzi wa kujaza nafasi zote zilizowazi na kama watataka kumrejesha Manji basi ni vyema wakamrejesha akiwa mdhamini au mwekezaji wa klabu hiyo

ADVERTISE HERE