Kiungo fundi Thabani Kamusoko ambaye jana alipewa majukumu ya kukiongoza kikosi cha Yanga kama nahodha, amepongeza upambanaji ulionyeshwa na wachezaji wa Yanga kwenye mchezo wa ngao ya Jamii licha ya kupoteza mchezo kwa mikwaju ya penati dhidi ya Simba.
Kamusoko, Tshishimbi na Raphael Daudi walionesha ushirikiano mzuri katika nafasi ya kiungo huku Emanuel Martini na Ibrahim Ajib wakiisaidia timu wakitokea pembeni.
"Hatukufanikiwa kupata ushindi siku ya leo, lakini nimefurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na kila mmoja wetu," amesema.
"Hakika mafanikio yako mbele yetu, penati hazina mwenyewe."

Yanga itashuka dimbani Jumapili katika mchezo wake wa kwanza ligi kuu ya Vodacom, ikimenyana na Lipuli kwenye uwanja wa Taifa.

ADVERTISE HERE