Mzuka wa mashabiki unachangia ushindi wa Yanga - Tambwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Dec 2018
Mzuka wa mashabiki unachangia ushindi wa Yanga - Tambwe
Mshambuliaji wa Yanga Amisi Tambwe amesema miongoni mwa mambo yanayowafanya waipiganie timu hiyo mikoani ni idadi kubwa ya mashabiki wanaojitokeza kuwaunga mkono

Tambwe amefichua kuwa wamekuwa wakipata sapoti ya kipekee kutoka kwa mashabiki jambo linalowafanya wajihisi kuwa na deni kubwa kwao

"Hamasa wanayotupa mashabiki inatufanya tujitume zaidi ili tusiwaangushe. Ukiwa uwanjani unacheza na ukaona jukwaani kuwa mashabiki wengi sana wanakuunga mkono, utajiona kama una deni kwao," amesema Tambwe

"Ndio maana tumekuwa tukijitahidi kuhakikisha tunashinda kila mchezo ili kuwafurahisha mashabiki wetu"

Juzi Tambwe aliibeba Yanga kwa kuifungia mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Tanzania Prisons

Katika mchezo huo Tambwe alingia katika dakika ya 72 na kwa kiasi kikubwa ndiye aliyefanikisha ushindi wa Yanga kwani hata bao la mkwaju wa penati lililofungwa na Ajib mpira uliosababisha madhara ulianzia kwake

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 ameahidi kuendeleza rekodi ya kupachika mabao kadiri atakavyopewa nafasi na kocha Mwinyi Zahera
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’