Viongozi wa Yanga Mbeya waongeza mzuka wa kikosi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Dec 2018
Viongozi wa Yanga Mbeya waongeza mzuka wa kikosi
Leo Jumatatu jioni mabingwa wa kihistoria Yanga watashuka kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya kuikabili Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara.

Jana jioni viongozi wa Yanga wa mkoa wa Mbeya waliibuka kambini hotel ya FQ kuwaongezea mzuka wachezaji pamoja na benchi la ufundi kuelekea mchezo huo.

Kikosi cha Yanga kiko kamili tayari kwa mtanange huo unaosubiriwa kwa hamu na wakazi wa mkoa wa Mbeya na maeneo ya jirani

Yanga inayoongoza ligi ikiwa na alama 35 itakuwa na nafasi ya kujiimarisha zaidi kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kama itaibuka na ushindi katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali.

Kikosi cha Yanga kitaendelea kuwakosa baadhi ya wachezaji kutokana na majeraha na matatizo binafsi.

Gadiel Michael, Juma Mahadhi, Baruani Akilimali, Papi Tshishimbi, Kelvin Yondani na Beno Kakolanya ni miongoni mwa wachezaji watakaokosa mchezo huo
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’